Home Habari za michezo HUYU AZIZI KI MNAEMUONA NI ASILIMIA 40 TU

HUYU AZIZI KI MNAEMUONA NI ASILIMIA 40 TU

Habari za Yanga

Mchambuzi maarufu wa masuala ya soka nchini, George Ambangile amesema kuwa kiwango cha kiungo mshambuliaji wa Yanga, Aziz Ki anachokionesha kwa sasa ni asilimia 40 tu ya uwezo wake hivyo wasishangae kumuona anafanya makubwa zaidi ya anayofanya sasa.

Ambangile amesema hayo ikiwa ni baada ya Aziz kurejea msimu huu akiwa na moto wa kuisaidia zaidi timu yake kufunga na kutoa pasi za mabao karibu kila mechi anayocheza tofauti na msimu uliopita ambapo kiwango chake kilikuwa kikibadilika siku moja hadi nyingine na kusababisha Kocha Nabi kuwa anampiga benchi.

“Msimu uliopita nilihoji sana kuhusu fitness level ya Aziz, kuna wakati alionekana amefunga bandage kwenye goti lake hata lugha ya mwili wake ilikuwa inaonyesha hayuko fit. Wakati yupo ASEC Mimosas alikuwa na mwili mdogo na mwepesi, alikuwa sharp na haraka kufanya maamuzi na muda wote anautaka mpira.

“Alipokuja Yanga ilikuwa akituliza mpira unaona mtu anauchukua, ni kama alikuwa anaogopa kutonesha kitu kwenye mwili wake, alikuwa anaangakuka tu kila mara. Hata mashabiki ilikuwa akiwekwa benchi hakuna shabiki anayelalamika. Ukiangali mwili wake wa sasa na msimu uliopita, Aziz wa sasa ameanza kupungua mwili.

“Aziz amehisi kama ana deni kwa Yanga japo msimu ulipita hakufanya vibaya, amechangia kutenegeneza mabao zaidi ya 10. Sasa baada ya kuona usajili uliofanyika amehisi atapigwa benchi ameamua kufanya kazi ili kila mtu ajue uwezo wake uko vipi.

“Kwa hiki ambacho Aziz anakifanya na kipaji chake alicho nacho ni kama asilimia 40 tu. Nilimtazama Aziz akiwa ASEC mechi yao dhidi ya RS Berkane, alipiga soka si la kawaida, dribbling, kasi, uharaka, mashuti, ni ngumu sana kukabiliana naye na unaona huyu ni namba 10 unayehitaji kuwa naye,” amesema Ambangile.

SOMA NA HII  YANGA YAHOFIA KUFANYA MAKOSA KWENYE USAJILI, HESABU ZAO HIZI HAPA