Home Simba SC RAGE ATOA POVU KUUZWA KWA MIQUISSONE NA CHAMA,..AMTAJA OKWI

RAGE ATOA POVU KUUZWA KWA MIQUISSONE NA CHAMA,..AMTAJA OKWI


KIKOSI cha Simba ni bora. Hiyo ni kauli ya aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Simba Ismail Rage kwa timu yake akiamini itakuwa tishio zaidi ya msimu uliopita kutokana na maandalizi yanayofanyika kwa sasa.

Amesisitiza kwamba hata kuondoka kwa Clatous Chama na Luis Jose hakuwezi kuwa na athari kwani miaka yan nyuma waliwahi kuondoka kina Emanuel Okwi na Simba ikaendelea kutisha.

Msimu uliopita Simba ilichukua mataji yote matatu la Ngao ya Hisani, Ligi Kuu pamoja na Kombe la Shirikisho la Azam huku watani zao Yanga wakiambulia patupu.

Rage alisema hata kwenda kuweka kambi Morocco ni eneo sahihi kutokana na utulivu wao ambao wameuweka huko umezidi kuijenga zaidi timu yao chini ya Kocha Didier Gomes.

“Simba wako vizuri sana ina kikosi bora na kimekaa kwa muda hivyo sina wasiwasi na kikosi hicho najua kitafanya vizuri sana,”alisema Rage ambaye ni kiongozi wa zamani wa TFF.

Aidha Rage alisema, hata usajili umekuwa bora wamefanya kwa mahitaji sahihi na matakwa ya mwalimu hasa wachezaji wa Kigeni.

“Ukiangalia wachezaji walioingia ndani ya Simba kwa sasa una tija kubwa na wanasimba wasifikirie kuwa kuondoka kwa Luis Miquissone na Clatous Chama kuwa kutaifanya timu isifanye vizuri,”

“Simba ilikuwa na wachezaji wazuri na wakali akina Mogella, Ramadhan Mtemi, Rino na Gaga walikuwa moto hao bila kumsahau Okwi lakini waliondoka na Simba ipo inafanya vizuri mnoo,” alisema Rage na kuongeza Simba imekuwa bora muda mrefu.

SOMA NA HII  ISHU YA DEREVA WA SIMBA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUENDESHA GARI KINYUME NYUME ...UKWELI UKO HIVI...