Home Habari za michezo ISHU YA DEREVA WA SIMBA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUENDESHA GARI KINYUME NYUME...

ISHU YA DEREVA WA SIMBA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUENDESHA GARI KINYUME NYUME …UKWELI UKO HIVI…

Basi la Simba

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Ramadhani Ng’azi amesema, ikibainika dreva wa Simba aliyeendesha kinyumenyume alifanya kwa makusudi na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara, basi ataburuzwa mahakamani.

Kwa mujibu wa Kamanda Ng’azi, uchunguzi utafanyika kubaini sababu za Dereva wa Basi la Klabu ya Simba SC kuendesha gari hilo reverse (Kinyumenyume) kwa umbali mrefu.

Endapo itabainika kuwa alifanya kwa makusudi, atafikishwa Mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. Adhabu tajwa kufuatia kosa hilo inaweza kuwa Faini ya Tsh Elfu 20 za Kitanzania.

Inasemekana, dereva wa basi hilo alifanya tukio hilo wikiendi iliyopita wakati Simba SC ilipokuwa inavaana na Raja Casablanca katika dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar.

SOMA NA HII  BENCHIKHA ATANGAZA POINT 15 ZA UBINGWA SIMBA....WENYE TIMU HIZI MJIANDAE...