Home Habari za michezo BAADA YA KUICHAPA MAZEMBE…NABI AWAPA ‘MAKAVU’ WALIOKUWA WANAMSEMA KUWA NI KOCHA WA...

BAADA YA KUICHAPA MAZEMBE…NABI AWAPA ‘MAKAVU’ WALIOKUWA WANAMSEMA KUWA NI KOCHA WA LIGI KUU PEKEE…

Habari za Yanga SC

Kocha Mkuu wa Yanga Nabi amewachana baadhi ya waandishi wanaodai kuwa yeye ni wa Ligi Kuu tu, lakini Kimataifa hana makali yoyote kama anavyofanya vizuri NBC.

Baada ya kuwafunga TP Mazembe, Kocha Nabi akawauliza waandishi je ushindi mnono aliopata jana ni wa Ligi Kuu?

“Si mlikuwa mnasema Nabi hawezi kimataifa? Hii mechi ya leo sio ya kimataifa,” aliwahoji waandishi Nabi.

Yanga aliibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya TP Mazembe kwenye mchezo wa pili wa hatua ya makundi mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

Kufuatia ushindi huo, Yanga inakamata nafasi ya tatu kwenye kundi lao wakilingana na TP Mazembe.

Pia Jumatano, timu hiyo watashuka dimbani kukipiga na KMC kenye muendelezo wa Ligi Kuu ambapo huku wanaongoza msimamo wakifuatiwa na Simba.

SOMA NA HII  UONGOZI WA YANGA WAWAFARIJI WAATHIRIKA WA MAFURIKO HANANG......RAIS WA YANGA AFANYA HIVI