Home news FT: SIMBA 1-0 RS BERKANE…SAKHO AWASAKUA WAARABU…WATAKA KUZICHAPA KAVUKAVU UWANJANI…

FT: SIMBA 1-0 RS BERKANE…SAKHO AWASAKUA WAARABU…WATAKA KUZICHAPA KAVUKAVU UWANJANI…


BAO la pekee la  Pape Sakho lililofungwa dakika ya 44 ya mchezo lilitosha kuwatoa Simba kifua mbele kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkhane.

Sakho aliwatoka mabeki wawili ndani ya box na kukandamiza mpira ndani ya nyavu na kumuacha kipa Hamza Hamiani Akbi kukosa cha kufanya.

Mpira ulianza kwa kupooza huku timu zote zikisomana namna ya kushambuliana wenyeji Simba walionyesha nia  ya kuhitaji bao la kuongoza kutokaba na kuliandama lango la wapinzani wao mara kwa mara.

Simba walipata kona mbili kipindi cha kwanza zilizochongwa na Larry Bwalya hazikuwa na madhara langoni kwa wapinzani wake.

Dakika ya tatu na tano Simba walifanya mashambulizi langoni mwa RS Berkane kama sio umakini wa walinzi wa timu hiyo wangemaliza dakika za kipindi cha kwanza na mabao zaidi ya walilofunga.

Dakika ya 45 za kipindi cha kwanza Kanoute alimfanyia madhambi Adama Ba na kuonyeshwa kadi ya njano iliyozua taflani na kufanya benchi la ufundi la Simba kuingia ndani ya uwanja kumsaidia mchezaji wao aliyekuwa anazongwa na wapinzani.

Wakati huo huo benchi la RS Berkane pia liliingia uwanjani kutuliza vurugu zilizizokuwa zinaendelea huku wengine wakionyesha jitihada za kumsaidia Ba ambaye alitolewq uwanjani akichechemea.

Kipindi cha pili timu zote zilishambuliana kwa kasi huku washambuliaji wakikosa umakini kuweza kusukuma mpira kimiani.

Hata hivyo, RS Berkane walipata goli ambalo lilikataliwa na mwamauzi kwa kigezo cha kuwa mfungaji alikuwa ameotea kabla ya kufunga.

Tukio hilo lilizua tafrani kwa wachezaji na benchi la ufundi la RS Berkane,jambo ambalo kwa kiasi fulani liliufanya mchezo kusimama kwa zaidi ya dakika nane.

SOMA NA HII  WAKATI YA MHILU HAYAJAPOA...KOCHA GWAMBINA AIBUKA NA HILI KUHUSU STAA MPYA WA SIMBA