Home Azam FC MUDATHIR AVUNJA UKIMYA AZAM…AFUNGUKA KINACHOWAKWAMISHA..WACHEZAJI NA KOCHA WATAJWA..

MUDATHIR AVUNJA UKIMYA AZAM…AFUNGUKA KINACHOWAKWAMISHA..WACHEZAJI NA KOCHA WATAJWA..


KIUNGO wa Azam FC, Mudathir Yahya amekiri timu yao kupoteza muelekeo baada ya kushindwa kupata matokeo kwenye mechi tatu mfululizo huku akikiri kuwa kujiamini ndio kunawafanya washindwe kufanya kile wanachoelekezwa.

Azam, ilianza na kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Biashara United, ikatoka suluhu na Coastal Union na ikakubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania na leo wanashuka dimbani kumenyana na Namungo.

Mudathir alisema timu yao ina wachezaji wazuri na inaongozwa na kocha ambaye anatimiza majukumu yake vizuri shida ipo kwao wenyewe kujiamini kupitiliza bila kuwahofia wapinzani wao.

β€œSio rahisi kupoteza michezo mitatu mfululizo tukiwa tumetoka kwenye rekodi nzuri ya matokeo, shida ni kulewa kujiamini, tumejifunza kutokana na makosa, tutaendelea kupambana na kuwaheshimu wapinzani ili kuweza kufanya kilicho bora,” alisema na kuongeza;

β€œTunahitaji matokeo mazuri dhidi ya Namungo ili kuweza kurudi mchezoni bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwani tuna kikosi kizuri, wachezaji wenye uzoefu na wenye uchu wa mafanikio.”

Alisema wanawaheshimu wapinzani wao Namungo ambao watakuwa nyumbani lakini wao wamejiandaa kushinda ili kujiweka sawa kwenye msimamo wa ligi huku akiongeza kuwa bado wanaamini wanaweza kumaliza ndani ya nafasi tatu za juu kutokana na kuwa na michezo mingi.

SOMA NA HII  SIMBA KUPELEKA TUZO YAO YA CAF KWA HAYATI MAGUFULI....MPANGO MZIMA UKO HIVI..