Home Habari za michezo SIMBA KUPELEKA TUZO YAO YA CAF KWA HAYATI MAGUFULI….MPANGO MZIMA UKO HIVI..

SIMBA KUPELEKA TUZO YAO YA CAF KWA HAYATI MAGUFULI….MPANGO MZIMA UKO HIVI..

JPM

Tambo za Semaji la Wekundu wa msimbazi Ahmed Ally kueleka Chato Utalii Festival, amezungumza kuhusu walivyojiandaa.

Amesema wataipeleka Chato tuzo ya Mashabiki Bora waliyoipata hivi karibuni.

“Kutakuwa na michezo mbalimbali ambayo tutashiriki na sisi mashabiki wa Simba, tunaamini tutaenda kushinda!”

“Kubwa kabisa ni mpira wa miguu, mashabiki wa Simba na Yanga na hapo ndio eneo letu la kujidai lazima tuwafunge.”

“Mashabiki wa Simba tumekuwa bora sana na lazima tukathibitishe ubora wetu kwenye shindano kwa sababu mpaka tuzo tunayo na nitawapelekea watu wa Chato wakati tunacheza Tuzo ipo pembeni.”

SOMA NA HII  TWAHA KIDUKU: NGUMI ZANGU ZINAUMA