Home Habari za michezo KWA BALAA HILI LA PHIRI….ASIPOCHEZA KWA SIMBA HII YA SASA ASEPE TU...

KWA BALAA HILI LA PHIRI….ASIPOCHEZA KWA SIMBA HII YA SASA ASEPE TU KWENYE DIRISHA DOGO…

Habari za Simba

Mshambuliaji wa Simba, Moses Phiri huenda ameendelea kuwakosha Cadena na Matola na sasa wanafikiria kumuanzisha mechi na Asec Mimosas, Jumamosi hii.

Phiri mwenye mabao matatu hadi sasa kwenye ligi, juzi alifunga bao moja kati ya manne iliyoyapata Simba, kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Dar City iliyomalizika kwa ushindi wa mabao 4-0, huku mabao mengine yakifungwa na Che Malone Fondoh, Willy Onana na Israel Mwenda.

Cadena alisema maandalizi ya mechi hiyo yanaendelea vizuri na kila mchezaji aliyepo kambini anajituma na kumtaja Phiri kuwa na nafasi kubwa ya kucheza mechi ijayo.

“Nawapongeza wachezaji wangu kwa kiwango walichokionyesha. Mechi hiyo imetupa mwanga wa namna timu yetu ilivyo hususani muda huu ambao baadhi ya wachezaji hawapo. Tunachokifanya leo ni kuandaa timu itakayocheza mechi inayokuja. Kila mchezaji anayeonyesha kiwango bora akiwemo Moses (Phiri), anafaa kucheza mechi hiyo,” alisema Cadena.

Mastaa Kibu Denis, Aishi Manula, Chama na Henock Inonga wapo kwenye timu zao za taifa na wanatarajiwa kuwasili kambini kuanzia kesho Jumatano huku Shomari Kapombe, Ayoub Lakred, Luis Miquissone na Sadio Kanoute walikuwa na ruhusa maalumu wakitarajia kujinga na timu leo.

Kwa upande wake, Chama alisema kuwa: “Nitarudi Alhamis naamini tutarudi na nguvu tukianza mchezo wetu wa kwanza nyumbani nawaomba mashabiki wasahau yaliyipita tuungane kuipambania timu yetu pamoja;

“Mchezo wa soka una nyakati nzuri na mbaya tunatambua maumivu wanayoyapitia na sisi pia tunaumia tutarudi upya na kuipambania timu ili kufikia malengo.

SOMA NA HII  FEI TOTO HUKU AZAM NI MPYA KABISA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here