Home Habari za michezo UONGOZI WA YANGA WAWAFARIJI WAATHIRIKA WA MAFURIKO HANANG……RAIS WA YANGA AFANYA HIVI

UONGOZI WA YANGA WAWAFARIJI WAATHIRIKA WA MAFURIKO HANANG……RAIS WA YANGA AFANYA HIVI

Rais wa Club ya Yanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vilabu vya soka Barani Afrika (ACA) Injinia Hersi Said jana ametembelea eneo la mafuriko katika kijiji cha Katesh Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara na kutoa pole kwa Waathirika na kuwasilisha misaada.

Taarifa rasmi kwa Waandishi wa Habari imeeleza yafuatayo; “Kwa kuunga mkono wito wa Rais Samia kuelekeza misaada ya haraka Wilayani Hanang, kwa kuunga mkono pia jitihada za Watanzania mbalimbali katika kuwasaidia Waathirika, Club ya Yanga kwa kushirikiana na GSM Foundation tumechangia vitu vyenye thamani ya Tshs. 40,000,000 pamoja na kutoa fedha taslim shilingi milioni kumi (10,000,000) kupitia akaunti ya mfuko wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa”.

Msaada huo umepokewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga pamoja na Viongozi mbalimbali walioweka kambi Katesh kusaidia zoezi zima la uokozi.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA AIPA TAHADHARI YANGA KWA ZESCO