Home Habari za michezo SIO POA SIMBA NA MBINU CHAFU ZA WYDAD…..UONGOZI WATIA NENO

SIO POA SIMBA NA MBINU CHAFU ZA WYDAD…..UONGOZI WATIA NENO

Habari za Simba

Uongozi wa Simba, umesema kuwa, kikosi chao kitaingia uwanjani kucheza dhidi ya Wydad Casablanca, kwa tahadhari kubwa ili wafanikishe malengo yao ya kufuzu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana Desemba 9, mwaka huu huko nchini Morocco, ukiwa ni mchezo wa tatu wa Kundi B katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba hadi hivi wana pointi mbili katika kundi lao, ikiwa imetoka kupata sare michezo miwili waliyocheza dhidi ya ASEC Mimosas na Jwaneng Galaxy.

Akizungumza nasi, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema kikosi chao kimeingia kambini jana Jumatatu tayari kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Wydad Casablanca.

Ally alisema wanakwenda kucheza mchezo huo kwa tahadhari kubwa, kutokana na wapinzani wao Wydad Casablanca kupoteza michezo miwili mfululizo kwa kufungwa na Jwaneng Galaxy na ASEC Mimosas, hivyo watakapokutana nao watacheza kufa au kupona ili wapate ushindi na watulize presha ya mashabiki.

“Kikosi chetu kimerejea kambini hii leo (juzi) kuanza maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Wydad Casablanca, ni mchezo muhimu kwetu kupata ushindi.

“Tunafahamu Wydad Casabalnca imepoteza mechi mbili za mwanzo, lakini hii haitupi nafasi ya kwenda kichwa kichwa kwani Wydad ni sawa na Mnyama mkali aliyesinzia, huwezi jua ataamka saa ngapi na ataamkia kwa nani.

“Kikubwa sisi tunapaswa kujiandaa tukiamini tunakwenda kucheza na mpinzani mgumu tukimkuta bado amelala fresh tunapita nae tukimkuta ameamka tunakomaa nae,” alisema Ally.

SOMA NA HII  GAMONDI ATOA NENO HILI BAADA YA YANGA KUIKANDA MTIBWA SUGAR