Home Habari za michezo GAMONDI ATOA NENO HILI BAADA YA YANGA KUIKANDA MTIBWA SUGAR

GAMONDI ATOA NENO HILI BAADA YA YANGA KUIKANDA MTIBWA SUGAR

Habari za Yanga SC

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa kikosi chake kilipaswa kushinda bao nyingi dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wao wa Ligi wa uliopigwa jana Desemba 16, 2023 katika Dimba la Azam Complex, Chamazi.

Gamondi amesema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo huo ambapo Yanga waliibuka na ushindi wa bao 4-1 na kufikisha alama 24 kwenye msimamo wa Ligi nyuma ya Azam wenye alama 25 huku Azam wakiwa na michezo miwili zaidi.

“Nawapongeza wachezaji wangu kwa ushindi wa leo,Ila sijafurahishwa sana na wachezaji wangu haswa kipindi chae kwanza kwa kushindwa kuzitumia nafasi ambazo tulizitengeneza.

“Kipindi cha kwanza tumetengeneza nafasi za wazi 11 lakini tumeshindwa kuzitumia. Sio mbaya tumefunga mabao 4 lakini tulitakiwa kufunga magoli mengi zaidi. Narudi uwanja wa Mazoezi kuwafundisha wachezaji pale ambapo wanakosea Katika kuzitumia nafasi.

“Nafurahushwa na muendelezo wa mchezaji wangu Stephanie Aziz KI kwa kiwango bora ambacho anakionesha kwa sasa,na nilimwambia kipindi nakuja Yanga,Wewe ndio utakuwa mfungaji bora msimu huu kwasababu naujua uwezo wa Stephanie Aziz KI,” amesema Gamondi.

SOMA NA HII  SIMBA INAMTU HUYU MMOJA TU