Home news KUELEKEA MECHI DHIDI YA KAGERA..CHAMA AIBULIWA UPYA..KAGERE, BOCCO, WASOTA KWENYE MBAO NDEFU…

KUELEKEA MECHI DHIDI YA KAGERA..CHAMA AIBULIWA UPYA..KAGERE, BOCCO, WASOTA KWENYE MBAO NDEFU…


KIUNGO wa Simba Clatous Chama ameanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar unaopigwa katika uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Hii ni mara ya kwanza kwa kiungo huyo kuanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara tangu asajiliwe akitokea klabu ya RS Berkane ya Morocco ambapo katika mechi iliyopita dhidi ya Mtibwa Sugar aliingia kipindi cha pili na kucheza dakika 45.

Katika kikosi chake hakuna mshambuliaji aliyeanza huku akiwaweka benchi Meddie Kagere na John Bocco.

Kikosi kamili kinachoanza ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Joash Onyango, Henock Inonga, Sadio Kanoute, Pape Sakho, Mzamiru Yassin, Bernard Morrison, Clatous Chama na Larry Bwalya.

Wachezaji wa akiba ni Beno Kakolanya,  Israel Mwenda, Gadiel Michael, Kennedy Juma, Erasto Nyoni, Hassan Dilunga, Meddie Kagere, John Bocco na Yusuph Mhilu.

Simba inaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa na nafasi ya pili na pointi 25, huku kwa upande wa Kagera Sugar inashika nafasi ya 11 na pointi 13.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA WAANGOLA....DEWJI ATOA DILI TAMU KWA MASHABIKI SIMBA...