Home Yanga SC FEI TOTO: MAMBO MAZURI YANAKUJA MSIMU UJAO

FEI TOTO: MAMBO MAZURI YANAKUJA MSIMU UJAO


BAADA ya kukosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la FA, Kiungo mshambuliaji wa Yanga Feisali Salum ‘Fei Toto’ amefunguka na kuwataka mashabiki wa timu hiyo kutokata tamaa kwani wanaenda kujipanga ili kufanya vizuri msimu ujao.

Katika  msimu huu wa Ligi Kuu Bara alifanikiwa kuifungia timu yake ya Yanga   mabao matano na kutoa pasi moja ya bao.

Akizungumzia mipango yao, Feitoto amesema kuwa mashabiki wa timu yao wasikate tama kwani mambo mazuri yanakuja msimu ujao wanaendelea kujipanaga kurejesha furaha ya mashabiki wao.

“Tunawaomba mashabiki  wetu  wasikate tama  kwani mambo mazuri yanakuja waendelee kuwa pamoja na sisi, na tunawashukuru sana kwa sapoti wanayotuonyesha na tunawaahidi kufanya vizuri msimu ujao.

“Msimu huu hatujafanikiwa kufikia malengo yetu lakini hatuja kata tama tunaendelea kujipanaga ili kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi na kutimiza malengo yetu,”amesema Feisal.

SOMA NA HII  ALLY KAMWE:- TUNA OFA KWA AZIZI KI KUTOKA AFRIKA KUSINI, MOROCCO NA MISRI....