Home Taifa Stars STARS YAAHIDI UBINGWA FAINALI CECAFA U23

STARS YAAHIDI UBINGWA FAINALI CECAFA U23


BAADA ya kufanikiwa kutinga katika hatua ya fainali ya michuano ya CECAFA U23, nahodha wa kikosi cha Taifa Stars, Israel Mwenda amesema kuwa matuaini yao makubwa kwa sasa ni kuweza kurudi na kombe.

Tanzania baada ya kutinga katika fainali ya michuano hiyo watacheza na timu ya taifa ya Burundi Julai 31 Jumamosi huko nchini Ethiopia ambapo michuano hiyo ilikuwa inafanyika.

Tanzania imetinga hatua ya fainali mara baada ya kuifunga timu ya taifa ya Sudan Kusini kwa bao 1-0 huku Burundi wao wakiwatoa timu ya Kenya kwa mikwaju ya penati 4-2, mara baada ya timu hizo kutoka sare katika dakika 90.

Akizungumzia mipango yao, Mwenda amesema kuwa matarajio yao ni kuhakikisha wanarudi nyumbani wakiwa na kikombe hiko, hivyo watapambana katika mchezo wa fainali ili tuweze kuwa mabingwa.

“Tumedhamiria kuwa mabingwa wa michuano hii, tumefika fainali na tuna malengo ya kuwa mabingwa, kuhusu kurudi na kombe nyumbani pia tunatarajia kuona hilo likitokea, tunaomba maombi kwa watanzania wote.”amesema nahodha huyo.

SOMA NA HII  KUHUSU UNDANI WA STARS KUTOKA SARE NA ZAMBIA JANA....UKWELI USIOSEMWA HUU HAPA...