Home Habari za michezo HAYA HAPA YALIKUWA SEHEMU YA MAAJABU YA MWAMUZI WA YANGA vs SIMBA...

HAYA HAPA YALIKUWA SEHEMU YA MAAJABU YA MWAMUZI WA YANGA vs SIMBA JANA…

Mwamuzi Ramadhan Kayoko jana aliweka rekodi kwa mechi za dabi za hivi karibuni baada ya kugawa jumla ya kadi za njano tisa, wakati Simba na Yanga zilipopambana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Katika mechi hiyo, Kayoko aligawa kadi tano za njano kwa Simba na nyingine nne kwa Yanga katika pambano hilo la 109 katika Ligi ya Bara tangu mwaka 1965.

Wachezaji wa Simba waliopewa kadi hizo ni Israil Mwenda, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Mzamiru Yasin, Habib Kyombo na Augustine Okrah, wakati kwa Yanga waliolimwa ni Djuma Shaban, Stephane Aziz KI, Khalid Aucho na Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Ilikuwa ni miujiza tu kwa mwamuzi huyo kutoa kasi nyekundu kwa namna wachezaji wa timu zote walivyoonekana kukamiana na kuchezea ubabe katika dakika zote 90. Jonas Mkude angeweza kutolewa kwa kadi ya pili ya njano mapema kabla ya Fei Toto aliyekuwa na njano naye kucheza faulo ambayo ilistahili kadi ya pili ya njano.

Mechi iliyokuwa inashikilia rekodi kwa kadi nyingi za dabi lilikuwa ni lile la Mei 6, 2012 wakati Yanga ikipigwa mabao 5-0 ambapo mwamuzi Hashim Abdallah alitoa njano saba na penalti tatu na kuifanya Simba ikabidhiwe taji lao kwa shangwe.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI