Home Habari za michezo SIKU KADHAA TOKA AJIUNGE NA SINGIDA BIG STARS…NDEMLA AIBUKA NA HAYA MAPYA…AGUSIA...

SIKU KADHAA TOKA AJIUNGE NA SINGIDA BIG STARS…NDEMLA AIBUKA NA HAYA MAPYA…AGUSIA ISHU YA USAJILI ….


Kiungo mpya wa Singida Big Stars, Said Ndemla amesema amefurahishwa na mwanzo wa maisha mapya klabuni hapo ikiwamo maandalizi ya kikosi kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Ndemla alisema walianza kambi yao Dar es Salaam, wakiwa wanafanya mazoezi ya gym kabla ya kwenda Arusha walipo sasa ambapo muda mwingi hufanya mazoezi yale ya uwanjani.

Alisema licha ya timu hiyo kuwa ni mpya kwenye Ligi Kuu anatarajia watafanya vyema kwa sababu ina wachezaji wengi wenye uzoefu ambao wametoka katika timu mbalimbali kubwa hivyo kikosi chao kitakuwa bora msimu ujao.

“Timu ndio ni ngeni ila wachezaji wengi si wageni katika ligi, tuna uzoefu kutokana na kupita katika timu nyingine huko nyuma. Tumekutana pamoja hapa na nina imani tunakwenda kuonyesha ubora kwenye michezo ya ligi,” alisema Ndemla.

Aliongeza kwamba Arusha walipo wakati huu ni mahali pazuri kwenye utulivu kwa ajili ya kambi wanapata kila kitu wanachohitaji kwa wakati ili kuhakikisha benchi la ufundi na wachezaji wanafanya kile kilicho wapeleka huko.

“Ukiangalia timu yetu ilivyofanya usajili kila mmoja anatamani kuiona na hivyo hivyo kwa wapinzani ambao tutakutana nao watatupa ushindani wa kutosha.”

SOMA NA HII  BAADA YA KULIA LIA SAAANA...NABI AFUNGA MJADALA KUHUSU MAKAMBO KUTOCHEZA YANGA...