Home Habari za michezo KUELEKEA SIMBA DAY YA MWAKA HUU…MKUDE KUENDELEA KUWEKA REKODI HII YA KIPEKEE...

KUELEKEA SIMBA DAY YA MWAKA HUU…MKUDE KUENDELEA KUWEKA REKODI HII YA KIPEKEE NCHINI…


Kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude amesema anafurahi kuendelea kuweka rekodi ya kuwa mchezaji anayeshiriki matamasha mengi ya Simba Day ndani ya timu hiyo.

Mkude amefunguka hayo kuelekea siku ya Simba Day inayotarajiwa kufanyika Agosti 8 mwaka huu.

Kupitia mtandao wa kijamii Instagram ameandika kuwa ‘Agosti 8 tunaadhimisha Simba Day ya 14 kwangu mimi binafsi ni ya 12,”

“Ni heshima kwangu kuwa sehemu ya tamasha hilo kubwa la soka kwa miaka yote hiyo, tukutane kwa Mkapa kuadhimisha siku yetu wanasimba,” aliandika Mkude.

SOMA NA HII  KOCHA MPYA YANGA HUYU HAPA.....NABI ALITAKA KUSEPA NA FEI TOTO DILI LIKATIBUKA JIONIII...