Home Habari za michezo MUDATHIR AAIKA ISHU YA ‘KUTONGOZWA’ NA NABI…AFUNGUKA JAMBO LA MAYELE NA AZAM…

MUDATHIR AAIKA ISHU YA ‘KUTONGOZWA’ NA NABI…AFUNGUKA JAMBO LA MAYELE NA AZAM…

Habari za Yanga SC

Kiungo wa mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Bara, Mudathir Yahya amesema kuwa mara tu baada ya kuachana na mabosi wake wa awali, Wauza Ukwaju wa Dar, Azam FC, Kocha Mkuu wa Wanajangwani, Nasreddine Nabi alimpigia simu kumhitaji ajiunge na kikosi chake.

Mudathir  amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari baada ya kuisaidia timu yake hiyo kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu na Yanga kwa mara ya 29 juzi Jumamosi, Mei 13, 2023 katika Dimba la Azam Complex Chamazi huku akiweka kambani bao 2 katika bao 4-2 walizofunga Yanga dhidi ya Dodoma Jiji.

“Ni furaha kubwa kuchukua ubingwa nikiwa na Yanga, nilishawahi kuchukua nikiwa mdogo na Azam FC mwaka 2014, na leo nimechukua na timu kubwa nchini. Wachezaji wenzangu wananitania hasa Mayele ananiambia watanirudisha Azam ili nisichukue ubingwa tena.

“Kitu ambacho watu hawajui, wanadhani mimi nilitemwa na Azam, hapana. Mkataba wangu ulipoisha mimi na Azam tulishindwana kukubaliana kimaslahi, nikaamua kwenda nyumbani Zanzibar kupumzika kwanza.

“Kocha Nabi alinipigia simu akaniambia ananitaka nijiunge na kikosi chake, nikamwambia kwa sasa hapana, nataka nitulize kichwa kwanza lakini kama bado mtakuwa mnanihitaji nitakuja dirisha dogo, nilikaa nje miezi sita, Nabi alimisubiria baadaye nikajiunga na Yanga.

“Kila mchezaji wa Yanga amefanya kazi kubwa na sasa tunakwenda kujiandaa na mchezo wa pilibwa nusu fainali dhidi ya Marumo Gallants, tunaamini tutapambana na kupata matokeo, wachezaji waendelee kutusapoti, tunaitaka fainali na tunaamini kwa uweza wa Mungu tutafika,” amesema Mudathir.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO ...AHMED ALLY AFUNGUKA NAMUNGO WALIVYOWAPA 'SAPOTI' YA UBINGWA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here