Home Uncategorized SIMBA WAFUNGUKA JUU YA KUMSAJILI AJIBU WA YANGA

SIMBA WAFUNGUKA JUU YA KUMSAJILI AJIBU WA YANGA

UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa hauna haraka ya kufanya usajili kwa kuwa walikuwa wanasubiri ripoti ya mwalimu na tayari wameshaipata hivyo watatoa majibu kuhusu suala la usajili ikiwemo na suala la kumsajili nyota wa Yanga, Ibrahim Ajibu.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ amesema kuwa kwa sasa hawajafanya usajili wa mchezaji yoyote yule wa nje wala ndani kwa kuwa walikuwa wanasubiri ripoti ya kocha.

“Hakuna usajili ambao tumefanya kwa wachezaji wa ndani na wa nje, hata wale ambao mikataba yao imekwisha hakuna ambaye amesaini mkataba, tulikuwa tunasubiri ripoti ya mwalimu.

“Kwa sasa tayari tumeipata ripoti hivyo tunaanza kuifanyia kazi na tutajua kama ripoti inazungumza wachezaji gani wa kusajili tutawasajili na safari hii itakuwa ni mara mbili zaidi ya msimu uliopita, hivyo kuhusu Ajibu hatujamsajili,” amesema.

Ajibu amekuwa akihusishwa kujiunga na Simba msimu ujao baada ya mkataba wake na Yanga kukamilika jana huku dili lake la kujiunga TP Mazembe likiyeyuka.

SOMA NA HII  ARSENAL YAMTEMBEZEA CHARTOLN 6-0