Home Uncategorized SAMAKIBA ITADUMU MILELE

SAMAKIBA ITADUMU MILELE

NAHODHA wa timu ya Taifa, Mbwana Samatta amesema kuwa mpango wa kuisaidia jamii utakuwa ni wa kudumu kwa kuwa ni sehemu ya maisha kuwakumbuka wahitaji.

Samatta na Ali Kiba wameandaa mchezo maalumu wakiwa na kampeni yao inayokwenda kwa jina la nifuate na muunganiko wao unaitwa SAMAKIBA Foundation, Juni 2 watakuwa na mchezo uwanja wa Taifa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Samatta amesema kuwa lengo ni kuwakumbusha wenye uwezo kuwajali wengine wa kipato cha chini.

“Tumefanya hivi kwa ajili ya kuwakumbusha wale wenye kipato kikubwa kuwakumbuka wengine ambao kipato chao ni cha chini pamoja na kuwajali wahitaji, tulianza mwaka jana na mwaka huu tunaendelea na itakuwa ni kila mwaka,” amesema Samatta.
SOMA NA HII  SIMBA, YANGA, AZAM FC KUMJUA MBAYA WAKE LEO