Home Yanga SC BAADA YA KUACHANA NA YANGA….WAZIRI Jr AIBUKA NA HILI JIPYA..AMTAJA NABI

BAADA YA KUACHANA NA YANGA….WAZIRI Jr AIBUKA NA HILI JIPYA..AMTAJA NABI


Mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC na klabu ya Mbao FC, Wazir Junior amesema tatizo kubwa la wachezaji wa ndani kushindwa kuonesha uwezo ndani ya Simba na Yanga ni kwasababu ya kutoaminiwa.

Waziri Jr amesema hayo leo Agosti 24, 2021 kwenye Kipenga Xtra ya East Africa Radio inayosikika Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa 6:00 hadi 7:00 mchana.

”Ndani ya mechi 9 za kwanza nikiwa Yanga sikucheza, nilikuja kupata bahati kucheza mechi ya 10 ambayo ilikuwa dhidi ya KMC na ndio maana nikamwambia Makapu kuwa naenda kufunga leo na nikaandika ujumbe ule wa ”Mwamba wa CCM Kirumba” na kweli nikafunga” – Wazir Junior

Aidha Wazir Junior ameongeza kuwa, ”Changamoto kubwa ya vilabu vyetu ni kukosa watu wa saikolojia labda mpaka kocha aongee na wewe. Nashukuru kocha Nasreddine Nabi kwenye mechi ya Yanga Vs Simba SC aliniambia sababu za kutocheza na kesho yake nilikuwa wa kwanza kufika mazoezini” – Wazir Junior.

SOMA NA HII  KWA REKODI HIZI ZA JEMBE JIPYA KUTOKA MAZEMBE...YANGA ITAKUWA MOTO...MKATABA WAKE NI BALAA...