Home Yanga SC BREAKING: HAJI MANARA ATAMBULISHWA YANGA

BREAKING: HAJI MANARA ATAMBULISHWA YANGA


ALIYEKUWA Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara leo ametambulishwa ndani ya Yanga huku akiahidi kuwa tamasha la Jumapili la Wiki ya Mwananchi halijawahi kutokea. 


Manara amesema kuwa kazi anaanza kesho rasmi kwa kuzindua jezi mpya ambayo haina makando.
Utambulisho wa Haji Manara umefanyika leo katika ukumbi wa Hotel ya Serena katika mkutano wa Waandishi wa Habari ulioanza saa 12:58 jioni.

Akimtambulisha Senzo Mbatha ambaye ni Mshauri Mkuu kuelekea masuala ya mabadiliko amesema kuwa anarejea nyumbani na atafanya kazi kwa ushirikiano na wengine. 
SOMA NA HII  MAYELE AKUTANA KWA SIRI USIKU NA RS BERKANE...AWAMWAGIA SIRI ZA KUITUNGUA SIMBA LEO...