Home Yanga SC IMEFICHUKA: UKWELI JUU YA KAMBI YA YANGA KUVUNJWA HUU HAPA…TIMU YAMEGUKA

IMEFICHUKA: UKWELI JUU YA KAMBI YA YANGA KUVUNJWA HUU HAPA…TIMU YAMEGUKA


KIKOSI cha Yanga kimevunja kambi yake ya hapa jijini Marrakech nchini Morocco wakitaja sababu tatu za kuchukua uamuzi huo ambao umeonyesha kuwashtua wengi lakini wakakutana na Simba kwenye ndege.

Iko hivi. Yanga iliweka kambi hapa jijini Marrakech kuanzia Agosti 16 jioni ikipanga kujiandaa na maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabigwa Afrika ambapo awali kambi hiyo ilikuwa ifikie tamati Agosti 27.

Hata hivyo, juzi usiku ghafla ratiba hiyo ilisitishwa ikitanguliwa na vikao kadhaa vya makocha wakiongozwa na Nesreddine Nabi na mabosi wa klabu hiyo waliokuwa hapa.

Msikie Hersi

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Mhandisi Hersi aliwatangazia wanahabari kuwa wameamua kusitisha kambi hiyo kutokana na kumeguka kwa baadhi ya wachezaji wao ambao wanane kutakiwa kujiunga na timu za taifa.

“Ukiangalia tumeona timu itameguka hivi karibuni wachezaji wetu wasiopungua wanane wanatakiwa kwenda kujiunga na timu za taifa, utaona hapo tutabaki na wachezaji wachache sana hapa,” alisema Hersi.

Wachezaji wa Yanga ambao wameitwa timu za taifa ni wale watano wa Taifa Stars ambao ni kipa Ramadhan Kabwili, mabeki Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, viungo Feisal Salum na Zawadi Mauya.

Wengine ni viungo Mukoko Tonombe (DR Congo), Khalid Aucho (Uganda) na kipa Diarra Djigui (Mali) ambao wote wataondoka haraka kuwahi mataifa kambi ya mataifa yao.

Hersi ambaye pia Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM inayoidhamini na kuifadhili Yanga ameongeza kingine ni changamoto ya hali ya hewa hapa nchini Morocco huku na pia wanakabiliwa na ratiba ya mchezo wa wiki ya mwananchi na ule wa hatua ya awali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika pia vimewafanya kuchukua uamuzi huo.

“Tangu tufike hapa tumekuwa na changamoto ya hali ya hewa hapa Marrakech sasa kuna joto kali sana, sasa tumeona ni bora timu irudi nyumbani ambako hali yake ya hewa hata kama kutakuwa na joto lakini sio kama la huku.

“Tuna ratiba pia ya mechi ya wiki ya mwananchi ambayo itafanyika wiki hii mwishoni lakini pia mnajua kwamba tuna mechi ya hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa palepale nyumbani kwahiyo sababu hizi tumeiona ni bora maandalizi yetu yakafanyike palepale katika kumalizia.

SOMA NA HII  KWA YANGA HII WAPINZANI TUMBO JOTO, ALLY KAMWE ATAMBA

“Tulikuwa tuondoke hapa tarehe 27 lakini kuondoka kwetu leo kunatufanya sasa kuondoka kwa makundi mawili kundi la kwanza litaondoka leo (jana) na kufika nyumbani Tanzania kesho (leo) Jumanne mchana na kundi jingine litaondoka siku chache zijazo.”

Yanga itawasili nchini Tanzania leo mchana kwa kundi la kwanza ambalo litapitia Dubai lakini kundi jingine la wachezaji huenda likafika baadaye usiku likipitia Doha na Uturuki kulingana na tiketi zao.

Hata hivyo, baadhi ya wachezaji ambao walikuja pamoja na kundi lililopita Dubai wamelazimika kubaki wakikosa nafasi ambapo wataondoka Ijumaa mchana wakifika jijini Dar es Salaam Jumamosi mchana.

12 wabaki MOROCCO

Yanga imewaacha wachezaji 9 jijini Marrakech na daktari mmoja wa viungo na viongozi wawili ambao ndio wataondoka mwishoni katika kundi la mwisho.

Daktari wa viungo Yousseph Ammir jana alishuhudiwa  akisimamia ratiba ya kuendelea kujifua kwa wachezaji hao akiachiwa makaratasi na Nabi ambaye ameondoka jana.

USO KWA USO

Mastaa wa Yanga akiwamo kipa mpya Djigui, Aucho na Fei Toto, walikutana uso kwa uso kwenye uwanja wa ndege wa Morocco na nyota wa Simba wakiwamo kina John Bocco, Taddeo Lwanga na wakapanda ndege moja kurejea Bongo.

Mastaa wa Simba ambao waligongana katika ndege moja na wenzao wa Yanga jana ni pamoja na wachezaji 8 ambao wanakwenda kuitumikia Taifa Stars ambao ni kipa Aishi Manula, mabeki Israel Mwenda, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Kennedy Juma, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.

Wengine ni viungo Mzamiru Yassin, Thadeo Lwanga (Uganda) na mshambuliaji John Bocco huku kundi lingine likibaki nchini Morocco jijini Rabat wakiendelea kujifua na mazoezi.