Home news KWA REKODI HIZI ZA JEMBE JIPYA KUTOKA MAZEMBE…YANGA ITAKUWA MOTO…MKATABA WAKE NI...

KWA REKODI HIZI ZA JEMBE JIPYA KUTOKA MAZEMBE…YANGA ITAKUWA MOTO…MKATABA WAKE NI BALAA…

 


REKODI za winga mpya wa Yanga, Chico Ushindi zinatisha jambo ambalo linaonesha ni kweli timuhiyo imepata jembe la maana ambalo litakuja kuongeza makali katika safu ya ushambuliaji ambayo kwa sasa inazidi kuwa kiwembe.

Yanga tayari imekamilisha usajili wa mkopo wa winga huyo ambaye alikuwa anakipiga katika Klabu ya TP Mazembe ya nchini DR Congo.

Katika mkataba huo, kuna kipengele cha nyota huyo anayetumia miguu yote kusakata kabumbu kujiunga na Yanga moja kwa moja kama wataridhika na uwezo wake au kumuuza kisha fedha wagawane na TP Mazembe.

Ushindi ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 25, anamudu vema kucheza nafasi zote za mbele akiwa anacheza winga ya kulia na kushoto, lakini pia anaweza kucheza kama mshambuliaji wa kati namba 9 na wa pili namba 10.

Raia huyo wa DR Congo ambaye alijiunga na TP Mazembe msimu wa 2017/18, amefanikiwa kuichezea timu hiyo michezo 72 katika misimu minne na kuhusika kwenye mabao 47, akifunga 30 na kutoa asisti 17.

Pia amefanikiwa kuitumikia timu ya taifa ya DR Congo katika michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN) iliyofanyika mwaka huu nchini Cameroon ambapo alifunga mabao mawili na kutoa asisti moja.

SOMA NA HII  KMC WANAHESABU NDEFU MSIMU MPYA 2021/22