Home Uncategorized ISHU YA LAMINE MORO KUPIGWA SINDANO ZA GANZI IPO HIVI

ISHU YA LAMINE MORO KUPIGWA SINDANO ZA GANZI IPO HIVI

 


SHECKY Mngazija, daktari wa Klabu ya Yanga amesema kuwa nyota wao Lamine Moro huwa hapigwi sindano za ganzi ili aweze kucheza kwa kuwa yupo fiti ila kitu ambacho humkuta ndani ya uwanja ni sehemu ya mchezo.


Nyota huyo ambaye amekuwa mhimili mkubwa ndani ya kikosi hicho amefunga jumla ya mabao manne na kutoa pasi moja ya bao.

 Kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara uliopita wakati wakishinda mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji, beki huyo alionekana kutokuwa fiti jambo ambalo lilizua mjadala kwamba anasumbuliwa na majeraha ila anachezeshwa akiwa amepigwa sindano.

Daktari huyo amesema:”Lamine yupo fiti na hana majeruhi ambayo yanamsumbua pia hachezeshwi akiwa amepigwa sindano kwa sababu kanuni haziruhusu suala hilo.

“Kinachotokea ndani ya uwanja ni sehemu ya mchezo kwa sababu kila mchezaji anapambana kusaka ushindi kwa ajili ya timu yake jambo ambalo linamfanya naye awe kazi akisaka ushindi,” amesema.
SOMA NA HII  WAWA AYAKUBALI MAJEMBE HAYA MAWILI YA KAZI