Home Uncategorized WANA KINO BOYS KAMILI GADO KUIVAA JKT TANZANIA

WANA KINO BOYS KAMILI GADO KUIVAA JKT TANZANIA



UONGOZI wa Klabu ya KMC  wana Kino Boys umeweka wazi kwamba upo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya JKT Tanzania utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma.


KMC imekuwa kwenye mwendo wa kusuasua ambapo kwenye mechi zake tatu za hivi karibuni imeshindwa kusepa na pointi tatu ndani ya uwanja.


Mchezo wake uliopita ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Ihefu jambo ambalo limewaongezea hasira ya kupambana kupata matokeo.


Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa:-“Hali ya kikosi kwa ujumla iko vizuri, pamoja na kwamba tulipoteza mchezo wetu dhidi ya Ihefu lakini bado tunamatumaini makubwa ya kupata ushindi kwenye mchezo wetu unaofuatia, zaidi pia tunayafanyia kazi makosa ambayo yalifanyika katika mchezo wetu uliopita.


 “Kikubwa ni kwamba tunawaheshimu wapinzani wetu, hakuna timu nyepesi katika mchezo, ndio maana tumekuja hapa kufanya maandalizi yetu ya mwisho ambayo yatatuwezesha sisi kuondoka na alama tatu licha ya kwamba tunacheza ugenini, lakini mpira hauna ugeni kikubwa ni kujipanga tu.


Disemba 19 mwaka huu, KMC FC ilicheza na Timu ya Ihefu katika uwanja wa Highland Estate Ubaruku, ambapo awali pia ilicheza na Simba katika uwanja wa Mkapa, Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro na hivyo kupoteza michezo yote.


SOMA NA HII  OFISA HABARI WA SIMBA AREJESHA SHUKRANI KWA MASHABIKI NA WACHEZAJI