Home Uncategorized SIMBA: MCHEZO UTAKUWA MGUMU ILA TUPO TAYARI

SIMBA: MCHEZO UTAKUWA MGUMU ILA TUPO TAYARI


 UONGOZI wa Simba umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum ambao unatarajiwa kuchezwa Desemba 23, Uwanja taifa wa Zimbabwe.


Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kutokana na umuhimu wake huku Simba ikiweka wazi kwamba imejipanga kupata matokeo chanya. 


Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa maandalizi ambayo wameyafanya yanawapa matumaini ya kuweza kupata matokeo ambayo wanayafikiria.

“Kikosi kipo imara na maandalizi yanakwenda vizuri huku na tunaamini kwamba kwa namna ambavyo tumejipanga tuna nafasi ya kupata matokeo.

“Kikubwa mashabiki wazidi kutuombea na kutupa sapoti ili tuweze kushinda mchezo wetu, benchi la ufundi linatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu na wenye ushindani ila tupo tayari,” .

Mchezo huo utachezwa majira ya saa 9:00 kwa saa za Zimbabwe ambapo kwa Bongo itakuwa saa 10:00 jioni. 

SOMA NA HII  VIDEO:MRUNDI ANAYEKIPA SIMBA QUEENS ATAJA AMBACHO ANGEKIFANYA NJE YA SOKA