Home Uncategorized AZAM: TUNA OFA NYINGI ZA WACHEZAJI

AZAM: TUNA OFA NYINGI ZA WACHEZAJI

 


UONGOZI wa klabu ya soka ya Azam umekiri kupokea ofa nyingi za wachezaji wao kutoka timu mbalimbali za nje na ndani ya nchi.

Jana Jumapili Azam ilikamilisha mauzo ya mchezaji wake raia wa Cameroon, Alain Thierry Akono Akono kuelekea nchini Malaysia, ambapo nyota huyo anakuwa mchezaji wa tatu kuuzwa na Azam msimu huu baada ya Mshambuliaji,  Shaaban Idd Chilunda na kiungo mkabaji Novatus Dismas waliouzwa mwezi Oktoba.

Akizungumzia biashara hiyo ya wachezaji Mkuu wa Kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ amesema: “Baada ya kukamilisha usajili wa, Alain Akono kumekuwa na maswali mengi kuhusu ofa za wachezaji wa klabu yetu kwa kuzingatia huyu ni mchezaji wa tatu tumemuuza msimu huu baada ya Shaaban Chilunda na Novatus Dismas.

“Ni kweli tuna ofa nyingi kutoka ndani na nje ya nchi ambapo kuna baadhi ya klabu zinawahitaji kwa mkopo, na wengine moja kwa moja hivyo nasi tunafanya tathimini na kama kuna klabu itakidhi vigezo basi tutawatangaza hivi karbuni,”

SOMA NA HII  NYOTA SIMBA APATA OFA YA KUKIPIGA NCHINI ETHIOPIA