Home Habari za michezo PAMOJA NA KUANZA KUTUPIA SIMBA SC…NTIBAZONKIZA AWACHANA WANAYANGA…

PAMOJA NA KUANZA KUTUPIA SIMBA SC…NTIBAZONKIZA AWACHANA WANAYANGA…

Habari za Simba

Baada ya kuanza kwa kishindo ndani ya Simba SC akifunga mabao matatu ‘Hat trick’ na kutoa pasi ya bao ‘asisti’ moja Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’ amesema huu ni mwanzo tu utamu unakuja.

Saido juzi alianza kwenye kikosi cha kwanza cha Simba SC kilichoichapa Prisons mabao 7-1 kwenye Dimba la Mkapa, akipangwa safu ya ushambuliaji na mafundi wengine kama Clatous Chama, Pape Sakho na nahodha John Bocco na kunogesha eneo lile kiuchezaji ikiwa ni mechi yake ya kwanza tangu asajiliwe kwenye dirisha dogo hili akitokea Geita Gold na kuwaongoza Wanamsimbazi hao kupata ushindi huo ,mnono.

Nyota huyo anayeichezea pia timu ya taifa ya Burundi, amesema kuwa amefurahishwa na kuanza kwa kufunga na kuasisti, huku akiweka wazi huo ni mwanzo tu wa mengi aliyowaandalia Wanasimba yanakuja.

“Nimefurahi kuanza hivi, ni mwanzo mzuri ambao nimeufurahia sana na naamini kwa mwendo huu nitafanya mazuri zaidi huko mbele,” alisema Saido aliyeichezea Yanga kwa mafanikio msimu uliopita.

Aidha Saido alizungumzia muunganiko wake na wachezaji wenzake wa Simba SC kuwa moja ya maeneo anayoyaona yataisaidia timu kwenye kufikia malengo zaidi.

“Nawashukuru benchi la ufundi kwa kuniamini na kunipa nafasi, wachezaji wenzangu kwa kucheza kwa ushirikiano mkubwa na kuipa timu ushindi.

“Nimefurahia mchezo na naamini kadiri siku zinavyokwenda tutazidi kuzoeana zaidi na wachezaji wenzangu kiuchezaji na tutatengeneza timu imara ambayo itawapa furaha mashabiki wetu.” alisema Saido.

Mabao matatu aliyoyafunga juzi yamemfanya afikishe mabao saba kwenye ligi, huku ile asisti ikimfanya kuwa na pasi saba za mabao sambamba na Ayoub Lyanga wa Azam wote wakiwa nyuma ya Chama mwenye nazo 11.

Kocha Prisons afunguka:

Kocha wa Prisons, Patrick Odhiambo raia wa Kenya, ameukubali mziki wa kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Saido Ntibanzonkiza ’Saido’akisema ni bonge la mchezaji na mwenye maamuzi sahihi ndani ya uwanja.

SOMA NA HII  YANGA NA MCHONGO HUU LIGI YA MABINGWA