Home KMC FC KMC WANAHESABU NDEFU MSIMU MPYA 2021/22

KMC WANAHESABU NDEFU MSIMU MPYA 2021/22


 UONGOZI wa KMC umeweka wazi kuwa hesabu zao kwa msimu wa 2021/22 ni kuweza kupata matokeo mazuri tofauti na msimu uliopita.

Kwa sasa kikosi kimerejea Dar baada ya kuweka kambi kwa muda pale mji kasoro bahari, Morogoro na kina maingizo mapya ya kutosha ikiwa ni pamoja na Miraj Athuman ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Simba,Awesu Awesu ambaye alikuwa ni mali ya Azam FC yupo hapo kwa mkopo.

Pia inaye beki mkongwe Hassan Kesi ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Mtibwa Sugar ila kwa sasa anaanza changamoto mpya ndani ya KMC.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa jambo kubwa ambalo wanahitaji ni kupata matokeo chanya msimu mpya.

“Maandalizi yanakwenda vizuri na kila mchezaji anahitaji kuona kila kitu ambacho kinapangwa kinapata majibu.

“Jambo la msingi kwa wakati huu ni kuendelea kuomba dua kwa mechi zetu tunaamini tutafanya vizuri,” .  

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO BAO 5 ZA YANGA ZINAVYOITESA SIMBA HADI LEO