Home Uncategorized RUVU SHOOTING YATUMA UJUMBE KWA DODOMA JIJI

RUVU SHOOTING YATUMA UJUMBE KWA DODOMA JIJI

 


UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa utapambana kusaka pointi tatu mbele ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara wa raundi ya tano.


Ruvu Shooting imetoka kulazimisha sare mchezo wake uliopita wa raundi ya nne ikiwa nyumbani baada ya kukamilisha dakika 90 bila kufungana na Biashara United, Uwanja wa Uhuru.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa sare waliyoipata sio mbaya kwao kwani walicheza kwa kiwango kikubwa ambacho mashabiki walioshuhudia waliweza kuona ukweli wa Barcelona ya Bongo.

“Wengi wanaisahau Ruvu Shooting kwenye ramani ya soka lakini ni moja ya timu ambayo inawatumia vizuri wazawa na wanacheza ule mpira wa pasi nyingi mithili ya Barcelona.


“Tumetoka kupata sare mbele ya Biashara United tunatambua kwamba ilikuwa mchezo mgumu kumalizana nao lakini tupo vizuri kwenye upande wa suala la kucheza mpira mzuri ndani ya uwanja ambao mashabiki wenyewe wanakubali.


“Ukiwa ugenini unacheza kwa kujiamini, tulicheza na Mtibwa Sugar mchezo wa kwanza tulimiliki mpira tukashindwa kupata matokeo sasa mbele ya Dodoma Jiji tutafanya vizuri, mashabiki wajitokeze kuona namna tutakavyowapa burudani,” amesema.


Ruvu itamenyana na Dodoma Jiji, Oktoba 2, Uwanja wa Jamhuri Dodoma kwenye mchezo wa raundi ya tano utakaopigwa makao makuu ya nchi.

SOMA NA HII  NYOTA POLISI TANZANIA APATA MUDA WA KUWA KARIBU NA MKE WAKE