Home Namungo FC NAMUNGO FC YATINGA ROBO FAINALI, LUSAJO ASEPA NA MPIRA WAKE MBELE YA...

NAMUNGO FC YATINGA ROBO FAINALI, LUSAJO ASEPA NA MPIRA WAKE MBELE YA JKT TANZANIA

 


MSHAMBULIAJI wa kikosi cha Namungo FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Moroco, Relliants Lusajo leo Mei 2 amesepa na mpira wake baada ya kutupia hat trick katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya JKT Tanzania. 

Mchezo huo wa hatua ya 16 bora, Namungo imesonga mbele hatua ya robo fainali kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya JKT Tanzania baada ya dakika 90 kukamilika.

Lusajo alianza kupachika bao la kuongoza dakika ya 24, la pili dakika ya 27 na msumari wa tatu ilikuwa dakika ya 43 na kuwafanya Namungo kuenda mapumziko ubao wa Majaliwa ukisoma Namungo FC 3-0 JKT Tanzania. 

Ni Mussa Said dakika ya 71 na Najim Magulu dakika ya 88 kwa penalti na kufuta machozi kwa timu hiyo ambayo imekuwa na mwendo wa kusuasua msimu huu.

Namungo inaungana na Yanga, Biashara United, Simba ambao ni mabingwa watetezi, Dodoma Jiji na Rhino Ranger kuwa miongoni mwa timu ambazo zimetinga hatua ya robo fainali.


SOMA NA HII  SERIKALI YAITAKA YANGA, NAMUNGO KUIGA MFANO WA SIMBA