Home Uncategorized YANGA HAWATAKI UTANI, WANAUTAKA UBINGWA WA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

YANGA HAWATAKI UTANI, WANAUTAKA UBINGWA WA LIGI YA MABINGWA AFRIKA



BAADA ya kupata nafasi ya kushiriki michuano ya  Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga imeweka wazi lengo lao ni kutwaa ubingwa huo msimu ujao.


Yanga imepata nafasi ya kushiriki michuano hiyo msimu ujao baada ya kumaliza ligi msimu uliopita ikiwa nafasi ya pili huku Tanzania ikiongezewa nafasi za uwakilishi kutoka nafasi moja hadi mbili.

Klabu hiyo imepanga kuitumia hafla ya harambee yake kubwa itakayofanyika Juni 15 mwaka huu kwaajili ya kushauriana na kuweka mikakati itakayoiwezesha kutimiza lengo hilo pamoja na mengine makubwa ya msimu ujao.

Yanga imeendelea kuwahimiza wadau wa soka hasa wapenzi na mashabiki wake kununua tiketi kwaajili ya kuhudhuria hafla hiyo iliyopewa jina la ‘KUBWA KULIKO’ kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na kuweka wazi lengo hilo kwa mara ya kwanza.

“Tunajiandaa kuchukua Kombe la Mabingwa Afrika mwakani. Tarehe 15 Juni tunakutana kupanga, kushauriana na kukusanya fedha kutimiza lengo hilo na mengine makubwa msimu ujao na miaka ijayo,” imeeleza sehemu ya taarifa iliyotolewa na Yanga kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kiingilio katika hafla hiyo ni shilingi 50,000 au 100,000 kwa mtu mmoja, shilingi 1,000,000 kwa meza ya watu 10 (VIM), shilingi 5,000,000 kwa meza ya watu 10 (VIP) na shilingi 10,000,000 kwa meza ya watu 10 (VVIP). Pia itakuwa mubashara kupitia Azam Tv.

SOMA NA HII  DOZI YA SIMBA AFRIKA KUSINI NI MOJA MARA MBILI