Home Uncategorized ASTON VILLA WANAKUJA HIVI WANAKATAA, WAINYOOSHA BAO 1-0 ARSENAL

ASTON VILLA WANAKUJA HIVI WANAKATAA, WAINYOOSHA BAO 1-0 ARSENAL


ASTON Villa inayoshiriki Ligi Kuu England imeanza kurejesha matumaini ya kubaki ndani ya Ligi hiyo baada ya usiku wa kuamkia leo kushinda bao 1-0 mbele ya Arsenal.

Timu hiyo ambayo mashabiki wengi wa Tanzania wanaifuatilia kutokana na nyota Mbwana Samatta anayeipeperusha bendera ya Tanzania kwenye ligi hiyo pendwa anakipiga ambapo jana alitumia dakika 72 uwanjani kabla ya kumpisha Keinan Davis.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na Mahmoud Ahmed Hassan maarufu kama Trezeguet dakika ya 27 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huku mashabiki wa Arsenal wakimshushia lawma nyota wao Pierre Emerick Aubameyang kwa kushindwa kutimiza majukumu yake.

Ushindi huo unaifanya Villa kufikisha pointi 34 ikiwa nafasi ya 17 huku vita ya kushuka ikiwa ni dhidi ya Watford na Bournemouth ambao wote wamecheza mechi 37 na pointi ni 34 hivyo ili kujihakikishia nafasi ya kubaki inatakiwa ishinde mchezo wa mwisho dhidi ya West Ham United utakaopigwa Julai 26.

Arsenal iliyeyusha dakika zote 90 bila kupiga shuti ambalo lililenga lango la Aston Villa kwenye mchezo huo ambao Villa walipiga mashuti matatu licha ya kuwa na umiliki wa chini ambao ni 39 huku Arsenal wakiwa na umiliki wa asilimia 61.

SOMA NA HII  CORONA YAMTIBULIA MIPANGO HASSAN DILUNGA