Home Uncategorized CORONA YAMTIBULIA MIPANGO HASSAN DILUNGA

CORONA YAMTIBULIA MIPANGO HASSAN DILUNGA


HASSAN Dilunga, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa janga la Corona limetibua mipango mingi ambayo ilibidi iendelee.

Kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa Machi 17 na Serikali kupitia kwa Wazir Mkuu, Kassim Majaliwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona Dilunga alikuwa kwenye ubora wake.

Simba ikiwa imefunga mabao 63 amehusika kwenye mabao tisa akifunga sita na kutoa pasi tatu za mabao.

Dilunga amesema: “Mambo mengi yamebadilika na kwenda vile ambavyo hatukutarajia lakini hakuna namna ni lazima tahadhari ichukuliwe na wakati ukifika mambo yatakuwa kama ambavyo tulikuwa tumezoea.”

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA AITOA TIMU YAKE KWENYE MICHUANO YA KIMATAIFA