Home Uncategorized KOCHA SIMBA AITOA TIMU YAKE KWENYE MICHUANO YA KIMATAIFA

KOCHA SIMBA AITOA TIMU YAKE KWENYE MICHUANO YA KIMATAIFA

PATRICK Aussems, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba ambaye alipigwa chini akiwa ameiongoza timu hiyo msimu huu wa 2019/20 kwenye mechi 10 amesema kuwa itakuwa ngumu kwa Klabu ya Simba kuvunja rekodi ya kutinga hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Aussems, raia wa Ubelgiji alipokuwa na Simba aliifikisha kwenye hatua hiyo ya robo fainali jambo analoamini kuwa itakuwa ngumu kwa timu hiyo kufika kwa wakati huu.

” Malengo yao najua  ni kuona wanafanikiwa kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao na hilo lipo mikononi mwao kwani wanaongoza ligi wakiwaacha wapinzani wao lakini kufikia hatua ya robo fainali itakuwa ngumu.

“Ninajua  haliwezi kutokea kwa sababu siasa za viongozi na kila mmoja atahitaji kuona cha kwake ndiyo sahihi na ugumu wa michuano kimataifa kwa timu zenye malengo upo wazi ila siyo Simba,” amesema.


Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 71 kibindoni imecheza mechi 28 huku Azam FC inafuata nafasi ya pili na pointi 54 zote zimecheza mechi 28.

SOMA NA HII  WACHEZAJI MSIBWETEKE, TIMU ZITUMIE MAPUMZIKO HAYA KUYAFANYIA KAZI MAKOSA