Home Habari za michezo BARBARA GONZALEZ WA CHELSEA AJIUZULU …BILIONEA MPYA ATAJA KUWA CHANZO…BOSI MWINGINE NAYE...

BARBARA GONZALEZ WA CHELSEA AJIUZULU …BILIONEA MPYA ATAJA KUWA CHANZO…BOSI MWINGINE NAYE AKIMBIA…


Mkurugenzi wa Chelsea, Marina Granovskaia ameachia ngazi wadhifa wake baada ya kudumu Stamford Bridge kwa muda wa miaka 12.

Marina anafuata nyayo za Mwenyekiti wa klabu hiyo Bruce Buck, aliyetangaza kustaafu na atakiachia kiti chake alichodumu nacho kwa muda wa 19. Aidha bosi huyo mkongwe wa muda mrefu atabaki kuwa mshauri mkuu wa klabu.

Mabadiliko hayo ya uongozi yametokana na ujio wa bilionea mpya Todd Boehly, aliyenunua klabu Chelsea baada ya kupigwa bei na Roman Abramovich.

Marina alikuwa miongoni mwa viongozi aliyefanya mambo makubwa ndani ya klabu, lakini sasa safari yake inalekea kufika ukingoni kwa mujibu wa taarifa.

Katika mahojiano mbali mbali na vyombo vya habari nchini, Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez mara kadhaa amekuwa kinukuliwa kuwa Bi Mariana ni role model wake kwenye uongozi wa Soka, ambapo mara kadhaa amekuwa akiiga mambo mazuri kutoka kwake.

SOMA NA HII  BAADA YA KUSAJILIWA NA KUTOONEKANA...YANGA WAIBUKA NA KUANIKA ALIPO BEKI WAO MPYA..