Home Habari za michezo RASMI…BARBARA AANIKA SABABU ZA SIMBA KUMKOSA ADEBAYOR…ADAI WALITUMA OFA MARA TATU WAKAZIDIWA…

RASMI…BARBARA AANIKA SABABU ZA SIMBA KUMKOSA ADEBAYOR…ADAI WALITUMA OFA MARA TATU WAKAZIDIWA…


Kwa mara ya kwanza, CEO wa Simba SC, Barbara Gonzalenz amekiri kuwa, walimtaka sana nyota kutoka Nigeria, Victorien Adebayor lakini walizidiwa ofa na RS Berkane.

Barbara amesema kwenye kipindi hiki cha usajili, wamekuwa wakikutana na changamoto ya wachezaji kupandiwa dau kwani vilabu vingi vimekuwa vikiwafatilia wachezaji ambao wanawahitaji.

“Sasa hivi wakiona mchezaji tunamhitaji, nao wanakuja wanaweka ofa zao hivyo mchezaji anapanda thamani. Adebayo tulimtaka, tukapeleka ofa mara tatu na mwishoni tukazidiwa na Berkane,” alisema Barbara.

Mpaka sasa, Simba tayari wametangaza kumsajili Mosses Phiri raia wa Zambia na kuachana na nyota wao wawili, Rally Bwalya na Pascal Wawa.

SOMA NA HII  KISA SARE YA YANGA JANA...PABLO AANZA KUTABASAMU SIMBA...ADONDOSHA MAOMBI MAZITO WAZIDI KUPOTEANA...