Home Uncategorized SIMBA YENYE MAUMIVU YAIFUATA MTIBWA SUGAR YENYE HASIRA

SIMBA YENYE MAUMIVU YAIFUATA MTIBWA SUGAR YENYE HASIRA

Verified

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba leo wameanza safari kuelekea Morogoro kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar unataotarajiwa kuchezwa kuchezwa Februari 11,2020.

Simba ina maumivu ya kupoteza mchezo wao mbele ya JKT Tanzania imeifuata Mtibwa Sugar yenye hasira za kufungwa na Lipuli.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Timu, Patrick Rweyemamu amesema kuwa wachezaji wapo safarini kuifuata Mtibwa.

“Kikosi kimeanza safari kwenda mkoani Morogoro, kila kitu kipo sawa na wachezaji wana morali kubwa,” amesema.

Simba imetoka kupoteza mchezo wake mbele ya JKT Tanzania kwa kufungwa bao 1-0 itacheza na Mtibwa Sugar iliyotoka kupoteza mbele ya Lipuli kwa kufungwa bao 1-0.

SOMA NA HII  OLE GUNNAR AMWAMBIA SANCHO KABLA DIRISHA LA USAJILI HALIJAFUNGWA ATAIBUKIA UNITED