Home Uncategorized GUARDIOLA ISHU YA STERLING, ANAFIKIRIA KINOMA

GUARDIOLA ISHU YA STERLING, ANAFIKIRIA KINOMA


RAHEEM Sterling nyota wa Manchester City leo atakosekana kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya West Ham.

Nyota huyo ameumia nyama za paja na inasemekana kuwa huenda pia akakosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.

Pep Guardiola, Kocha Mkuu wa City amesema kuwa ni pigo kubwa na anafikiri ni miongoni mwa wachezaji waliowaweka kwenye wakati mgumu.


“Sterling ameumia na daktari ameshatuelekeza, nafikiri ngoja tuone lakini anaweza kurejea kabla ya mchezo dhidi ya Real Madrid,” amesema.

SOMA NA HII  VIDEO: MWANA FA AMTUMIA NAMNA HII MWAKINYO