Home Habari za michezo JEMEDARI SAID AIKAANGA TENA SIMBA…AFUNGUKA WATAKAVYOTESEKA MBELE YA WYDAD..

JEMEDARI SAID AIKAANGA TENA SIMBA…AFUNGUKA WATAKAVYOTESEKA MBELE YA WYDAD..

Habari za Simba

Mchambuzi wa Soka nchini, Jemedari Said Kazumari amesema kuwa Simba wanatakiwa kujipanga ili kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo wao wa Robo fainali dhidi ya Wydad Casablanca.

“Ni mechi ngumu sana kwa Simba, sio tu kwa sababu Wydad wana historia kubwa kwenye mashindano haya bali pia ni kulingana na kiwango chao cha sasa. Tumeona kwenye makundi wamecheza vizuri mpaka wakaongoza kundi lakini pia wachezaji wao wametoka kucheza nusu fainali ya Kombe la Dunia.

“Kwa Simba imehangaika sana msimu huu mpaka kuingia robo fainali kuliko misimu ya nyuma hata kwenye ligi hapa nyumbani wamekuwa wakisuasua sana lakini kwa mechi za hapa mwishoni ukiangali pamoja na ubovu wa Horoya lakini alikula 7-0, kwa hiyo kuna kitu unakiona Simba wameanza kukitengeneza.

“Hizi sio mechi za kutafuta alama, ni kutafuta kuvuka kwenda mbele bila kujali unafunga mabao mangapi. Ni namna ambavyo benchi la ufundi na wachezaji watakavyojiandaa. Waarabu wanapenda kujihami zaidi wakiwa ugenini lakini ukienda kwao utashambuliwa kama nyuki.

“Simba wamekwenda Morocco mara mbili, nah ii ni ya tatu sasa. Walikutana na RS Berkane wakafungwa, juzi wamefungwa na Raja Casablanca na sasa wanakutana na Wydad, kwa hiyo wanatakaiwa wajifunze ni wapi walikosea hizo mbili ili warekebishe hii ya sasa,” amesema Jemedari.

SOMA NA HII  HIKI HAPA KIKOSI CHA 'MAPRO' WA TZ WANAOWEZA KUTIKISA AFCON 2023 NA TAIFA STARS...