Home Habari za Yanga KAMWE:- SIMBA INA UONGOZI MAKINI NA IMARA…TUTAINGIA CHAKA…AWAPIGIA SALUTI WACHEZAJI SIMBA

KAMWE:- SIMBA INA UONGOZI MAKINI NA IMARA…TUTAINGIA CHAKA…AWAPIGIA SALUTI WACHEZAJI SIMBA

Habari za Yanga leo

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa wao kama Yanga wanaichukulia Simba SC kama timu tishio kwenye Ligi ya Tanzania na timu za Afrika Mashariki na Kati kutokana na ubora
wao.

Kamwe amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa
Habari na kuelezea Mipango ya Timu yake kuelekea katika Mchezo wa Derby ya Kariakoo Dhidi ya Simba SC Mchezo ambao utachezwa Aprili 20 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

“Hii mechi mpaka imekuwa dabi maan yake ina upekee wake, umuhimu wake na ugumu wake. Unapokwenda kwenye Dabi ya Kariakoo kwa mawazo ya kwamba umeshinda mechi nyingi, mshindani wangu ana hali mbaya, utaingia chaka.

“Sisi kama Yanga hatuitazami Simba kama mnavyoitazama, sisi tunaitazama Simba kama timu tishio (giant) tunayowania nayo ubingwa kwa sababu wana nafasi ya kutwaa ubingwa. Simba ni timu yenye wachezaji wazoefu waliocheza mechi nyingi kubwa na tunaitazama Simba kama timu yenye viongozi makini.

“Ukiniambia nitaje timu zenye viongozi makini siwezi kuiacha Simba, wana viongozi wazoefu na wanajua mipango ya kupata matokeo kwenye mechi ngumu licha ya kwamba wanapitia wakati mgumu lakini wapo imara.

“Simba wanweza kusumbuka kwenye mechi ndogo lakini ikija suala la mechi kubwa, mentality inabadilika, wanacheza kwa intensity ya juu,” amesema Kamwe.

SOMA NA HII  KUELEKEA DABI YA KARIAKOO...JUA LA KESHO KUISHA NA MASTAA WA YANGA...SKUDU ATANGAZA RAHA ZAIDI...