Home Uncategorized YANGA YA KAZE KAZINI LEO KUTESTI MITAMBO

YANGA YA KAZE KAZINI LEO KUTESTI MITAMBO


KIKOSI cha Yanga leo Jumapili, Novemba 15 kitakuwa na kibarua cha kumenyana na African Lyon kwenye mchezo wa kirafiki.

Mchezo wa leo ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku ni maalumu kwa ajili ya kutesti mitambo ya timu hiyo kuelekea kwenye mechi zijazo za ligi.

 

Chini ya kocha wao Cedric Kaze raia wa Burundi,mwenye tuzo ya kocha bora Oktoba kitatoa burudani kwa mashabiki wake ambapo kiingilio ni buku tatu tu, (3,000) mzunguko na VIP ni 5,000.

 

Kambi ya Yanga ipo Kigamboni, Dar, huku ikiwa na nyota wachache kutokana na wengine kutimkia kwenye timu za taifa. Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, amesema, kuwa: “Kila kitu kipo sawa na wachezaji wana utayari kwa ajili ya mchezo wetu wa kirafiki.

 

“Kuhusiana na mechi hiyo ya kirafiki dhidi ya African Lyon, kocha Kaze mwenyewe ndiyo ameitaka na anajua juu ya malengo yake ambayo ameyapanga kuhusiana na nini atakachokiona kwenye mechi hii.”

SOMA NA HII  NYOTA WA SIMBA CHAMA MIKONONI MWA YANGA