Home Habari za Yanga KAMWE AWACHANA MASHABIKI YANGA…SIMBA WAHUSISHWA…AMEFUNGUKA HAYA

KAMWE AWACHANA MASHABIKI YANGA…SIMBA WAHUSISHWA…AMEFUNGUKA HAYA

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa wao kama Yanga wanaichukulia Simba SC kama timu tishio kwenye Ligi ya Tanzania na timu za Afrika Mashariki na Kati kutokana na ubora wao.

Kamwe amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari na kuelezea Mipango ya Timu yake kuelekea katika Mchezo wa Derby ya Kariakoo Dhidi ya Simba SC Mchezo ambao utachezwa Aprili 20 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.

“Hizo hadithi ambazo mpo nazo kwenye mitandao ya kijamii na magrupu ya WhatsApp kwamba tunakwenda kumpiga mtu bao 20, au bao nyingi, ninaomba mzibadilishe, focus yetu iwe kwenda kutafuta alama tatu.

Mwisho wa msimu hatutakuwa mabingwa kumpiga Simba bao 100, bali kwa kuwa na alama nyingi kuliko timu inayoshika nafasi ya 2.

“Alama tatu ndizo za muhimu zaidi, tukishinda bao 1-0, au 2-1 au 3- 2, alama tatu ndiyo muhimu zaidi. Mabao haya yatakuja tu kutegemea na yeye amemka vipi, wakijichanganya watakula nyingi.

Hata Novemba 5, mabao matano yalikuja tu lakini sisi ajenda yetu ilikuwa alama tatu, Simba akajichanganya akala mkono.

“Najua Wanayanga mnajiamini, mnaiamini timu yenu, twendeni kwa wingi kwa Mkapa, wachezaji wanwahitaji mno. Wiki hii tusiwafuate wachezaji mitandaoni, tuwaache wajiandae kutupa ushindi siku ya Jumamosi,” amesema Kamwe.

SOMA NA HII  KISA KAULI YA "TUNAOUMIA NI SISI"...MASHABIKI YANGA WAPIGWA MARUFUKU KUONGEA ONGEA OVYO...