Home Habari za michezo KUHUSU KUONDOKA ZAKE SIMBA…BENCHIKHA AVUNJA UKIMYA…AWATAJA VIONGOZI….

KUHUSU KUONDOKA ZAKE SIMBA…BENCHIKHA AVUNJA UKIMYA…AWATAJA VIONGOZI….

Habari za Simba leo

ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha ameleza sababu kubwa ya kuondoka nchini na kuachana na timu hiyo ni matatizo ya kiafya ya mke wake.

Amesema hali hiyo ilipeleka kushindwa kufanya kazi yake vizuri kwa kuwa akili yake haikutulia kutokana na hali ya kiafya ya mke wake huyo kuhitaji kuwa naye karibu.

Kocha huyo bado yupo nchini anakamilisha baadhi ya mambo na viongozi wa Simba na muda wowote anatarajiwa kuondoka nchini na kurejea kwao Algeria.

Benchikha amesema hana tofauti wala shida viongozi wa Simba, matatizo ya kifamilia yamekatisha malengo yake ndani ya klabu hiyo ikiwemo kutaka kuendelea kuwepo kwa msimu mwingine.

“Viongozi hata mimi nilipenda kumaliza msimu huu na kuendelea lakini matatizo ya mke wangu ya kiafya yamekatza safari na Simba, uwepo wa mbali na familia imekuwa ngumu kwangu na kupelekea kutofanya kazi vizuri na akili kutotulia.

Kabla ya  uongozi kuweza kuniruhusu na kutoendelea na kile nilichokipanga, nasikitika sikuweza  kutimiza malengo ikiwemo kucheza nusu fainali na hata kuchukuwa ubingwa kwa bahati mbaya hatukuweza kufika kwa sababu ya ubora wa Al Ahly,” alisema Benchikha.

Ameeleza kuwa kuondoka kwake hakuhusiani na kutofikia malengo hayo ya kucheza nusu fainali na kutwaa taji hilo, anaamini kuwa ipo siku atarejea Tanzania kukinoa kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi.

“Kipindi kifupi nilipokuwa Tanzania nimefurahi sana, Wanasimba wamenipokea vizuri na kujiona kuwa nyumbani, naipenda Simba na nitaishi nayo milele ndani ya moyo, ipo siku nitarudi na isije kuwa ajabu nikarudi tena Simba,” amesema Benchikha

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUPATA KAZI UARABUNI...ADEL ZRANE AENDELE KUANIKA MAPYA KUHUSU SIMBA...ADAI ANAJUA YOTE ...