Home Habari za michezo KISA SARE YA YANGA JANA…PABLO AANZA KUTABASAMU SIMBA…ADONDOSHA MAOMBI MAZITO WAZIDI KUPOTEANA…

KISA SARE YA YANGA JANA…PABLO AANZA KUTABASAMU SIMBA…ADONDOSHA MAOMBI MAZITO WAZIDI KUPOTEANA…


Sare ya Yanga dhidi ya Tanzania Prisons ni kama imemzindua Kocha Mkuu wa Simba SC Pablo Franco, ambapo ameweka wazi kuwa bado hajakata tamaa na ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa sababu kuna mechi nane zimebaki kabla ya kumaliza msimu.

Pablo amesema ingawa wapo  nyuma kwa alama 10 dhidi ya vinara lakini kwa kuwa bado kuna idadi kubwa ya mechi zimebaki lolote linaweza kutokea na hatujakata tamaa.

Pablo ameongeza kuwa baada ya kutoka sare na Yanga katika mchezo wa Aprili, 30 walijiweka katika mazingira magumu ya kutetea ubingwa lakini kutokana na ratiba kubana hata kwa wanaongoza lolote linaweza kutokea.

β€œKama nilivyowahi kusema huko nyuma mbio za ubingwa bado zipo wazi. Tupo nyuma kwa pointi 10 lakini kama wanaongoza wataendelea kudondosha pointi nasi tukishinda zetu tunaweza kutetea ubingwa,” amesema Pablo.

Akizungumzia mchezo dhidi ya Ruvu Shooting walioibuka  na ushindi wa mabao 4-1 Pablo amesema wamecheza vizuri na wachezaji walifuata maelekezo ingawa kipindi cha kwanza tulipoteza nafasi kadhaa za kufunga.

β€œKwanza nimefurahi kwa ushindi huu mnono, mchezo ulikuwa mzuri tumetengeneza nafasi nyingi kipindi cha kwanza lakini hatukuzitumia vizuri. Tulivyorudi cha pili tulijirekebisha makosa na kufanikisha ushindi huu,” amesema Pablo.

SOMA NA HII  DILI LA MAYELE KUTUA AFRIKA KUSIN LAMFIKIA 'PROFESA' NABI...NA HAYA NDIO MAJIBU YAKE....