Home Habari za michezo WAKATI AKITAJWA KUTUA SIMBA…GEORGE MPOLE KAWASIKILIZA WEE…KISHA AKATAJA HUKU ANAKOPENDA KWENDA…

WAKATI AKITAJWA KUTUA SIMBA…GEORGE MPOLE KAWASIKILIZA WEE…KISHA AKATAJA HUKU ANAKOPENDA KWENDA…


Mshambuliaji wa Timu ya Geita Gold ya mjini Geita amesema kuwa ndoto yake kubwa ni kuchezea timu zinazoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL) kwa kuwa ndio ligi yenye ushindani zaidi duniani.

Mpole amesema hayo katika mahojiano maalumu ikiwa ni siku chache baada ya kutangazwa kuwa mchezaji wa ligi kuu ya Tanzania bara kwa mwezi aprili.

“Natamani sana kucheza mpira Uingereza, kwa sababu ya staili ya uchezaji, navutiwa sana na hata mechi nyingi sana za ligi ya Uingereza huwa ninaziangalia, ni ligi yenye ushindani, ligi inayotazamwa sana duniani.

Ameongeza “Kuna vitu huwa naviangalia navifanyia kazi, wanavyocheza, kuna baadhi ya vitu ambavyo naona hata mimi naweza kufanya, ingawa siyo kwa asilimia kubwa wenzetu wameimarika zaidi, lakini kuna baadhi ya vitu nikiviangalia navifanyia kazi”.

Siku za hivi karibuni, straika huyo anayeongoza kwenye orodha ya wafungaji kwenye Ligi Kuu, amekuwa kwenye tetesi nyingi zinazomuhusiaha kutakiwa na vigogo wa soka la bongo, Simba na Yanga.

SOMA NA HII  BAADA YA KUNG'AA KWENYE MECHI ZA KIMATAIFA NA BIASHARA UNITED...REDONDO APATA SHAVU JIPYA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here