Home Uncategorized YANGA YAITWA MEZANI IPEWE MTUPIAJI HUYU

YANGA YAITWA MEZANI IPEWE MTUPIAJI HUYU


UONGOZI wa Namungo FC umesema kuwa iwapo Yanga inahitaji saini ya nyota wao Bigirimana Blaise ni suala la kuzungumza kwani inawezekana.

Imekuwa ikielezwa kuwa Yanga inahitaji kuboresha safu ya ushambuliaji na inahitaji kupata saini ya Blaise anayekipiga Namungo.

Blaise amefunga mabao 10 ndani ya timu hiyo iliyo nafasi ya tano ikiwa imefunga mabao 34 na ina pointi 50 kibindoni.

Ofisa Habari wa Namungo FC, Kidamba Namlia amesema kuwa wamekuwa wakiskia kuwa Blaise anahitajika na Yanga ila halijafika mezani suala hilo.

“Yanga hawajaja mezani na imekuwa ikielezwa kuwa wanahitaji saini ya Blaise kama ni kweli waje mezani tuzungumze,” amesema.

SOMA NA HII  MPANGO MKUBWA WA KUMALIZA LIGI KUU ENGLAND UPO NAMNA HII