Home Habari za michezo SINGIDA WAIKAZIA SIMBA ISHU YA PHIRI NA MIQUISSONE….

SINGIDA WAIKAZIA SIMBA ISHU YA PHIRI NA MIQUISSONE….

Habari za Simba leo

Singida Fountain Gate imeitupilia mbali ofa ya Simba kuwapa winga Luis Miquissone na Mosses Phiri ili wamnase kiungo Marouf Tchakei

Simba ilikuwa tayari kuwatoa mastaa wake hao wawili kwa Singida FG ikionyesha kuhitaji sana saini ya kiungo huyo raia wa Togo anayejua kuchezesha timu na hata kufunga.

Simba imekubaliana kila kitu na Tchakei kupitia meneja wake lakini mkataba wa kiungo huyo na Singida FG ndio umekuwa kikwazo.

Singida FG Imewaambia Simba haijafika kwenye kina cha pesa inachotaka na wala haiwahitaji Phiri na Miquissone

Ndani ya hilo Phiri mwenyewe amewasisitizia Simba kuwa hataki kutoka kwa mkopo na kama hawamtaki njia rahisi ni kusitisha mkataba huo.

SOMA NA HII  BAADA YA SIMBA KUTUA TZ...PABLO ATEMA NYONGO...APIGA MARUFUKU WACHEZAJI KWENDA KULALA...