Home Habari za michezo KUHUSU KUTUA SIMBA….MAROUF TCHAKEI AFUNGUKA DILI LILIVYOKUWA ….

KUHUSU KUTUA SIMBA….MAROUF TCHAKEI AFUNGUKA DILI LILIVYOKUWA ….

Tetesi za usajili Simba leo

MAMBO bado ya moto, kuhusiana na usajili, baada ya kuwepo kwa tetesi za kiungo wa Singida Fountain Gate, Marouf Tchakei kuhusishwa kutua Simba, mwenyewe amefunguka ishu nzima.

Tchakei amesema hashangazwi kuona taarifa hizo hasa kipindi cha usajili, alichosisitiza hajazungumza na timu yoyote anachofahamu ni mali ya Singida.

β€œNimepewa likizo ya wiki moja, nipo mapumziko hivyo mambo ya usajili siwezi kuyazungumzia hayo nawaachia viongozi ndio wenye uhalali na hilo,”amesema.

Ameongeza “Nina mkataba wa mwaka mmoja na nusu, hivyo ni makosa kuanza kuzungumza na timu ndio maana nasema viongozi ndio wenye uwezo wa kulizungumzia jambo hilo.”

Kiungo huyo msimu huu ameifungia Singida, mabao matano kwenye Ligi Kuu.

SOMA NA HII  YANGA KUWAFANYIA SAPRAIZI MASHABIKI ZAO LEO...CHICO, KOCHA WA SIMBA WATAJWA KUTAMBULISHWA...